Je unafahamu kuhusu Usimamizi wa Fedha katika Biashara yako?

Bestway Capital Management
2 min readMay 27, 2020

--

Moja kati ya elimu muhimu kwa kila mtu ambaye ameamua kufanya biashara ni elimu ya usimamizi wa Fedha. Fedha inahitaji usimamizi wa hali ya juu ili iweze kuongezeka na kutimiza malengo ulionayo katika biashara yako.

Unapokosa usimamizi mzuri kwenye masuala ya fedha inaweza kuzalisha matatizo kadha wa kadha katika biashara yako. Baadhi ya matatizo yanayoweza kutokea kwenye biashara yako kwasababu ya kukosa usimamizi mzuri wa fedha.

Unaweza kupata hasara katika biashara yako.
Unaweza kupunguza kiasi cha mtaji wako.
Unaweza kuingia kwenye mgogoro wa madeni.
Unaweza kushindwa kununua malighafi kwaajili ya uzalishaji.
Unaweza kupoteza thamani ya jina la biashara yako.
Unaweza kupunguza thamani ya ubora wa bidhaa zako.

Kuna matatizo lukuki ambayo yanaweza kujitokeza kwasababu ya kukosa usimamizi mzuri kwenye masuala ya fedha hivyo elimu ya masuala ya usimamizi wa fedha ni muhimu sana katika biashara yako.

Usimamizi wa fedha ni nini ?

Usimamizi wa fedha ni namna ya kusimamia mapato na matumizi katika biashara ili kutimiza lengo fulani.

Mapato ni fedha inayoingia katika biashara yako kupitia mauzo.

Matumizi ni fedha inayotoka katika biashara yako kupitia malipo.

Biashara yoyote ni lazima iwe na lengo (objective) ili uweze kuwa na ufanisi katika hiyo biashara. Huwezi kuwa makini katika biashara kama hujui unahitaji kutimiza nini.

Mpango kazi wa biashara ( Business Plan) ni kitu cha muhimu sana kwa kila mfanya biashara ambaye anataka kuleta mageuzi makubwa katika uchumi wake binafsi na jamii inayomzunguka.

Unapoweka kwenye matendo elimu ya usimamizi wa fedha inatakusaidia kutimiza malengo uliyonayo katika biashara yako.

Jifunze zaidi kuhusu Usimamizi wa fedha na uwezekaji kupitia kiunganishi hikihttps://www.bcmholdings.io/

--

--

Bestway Capital Management
Bestway Capital Management

Written by Bestway Capital Management

Capital Management | Asset Management | Blockchain Based Innovation | Financial Markets Trading Academy | #WeTurnYourInvestmentIntoSecureProfit |

No responses yet